Askofu amshauri Mswati III kuachia madaraka

Tuesday 15 November 2011

Warembo bikra wakiwa wamejipanga ili Mfalme ajichagulie mchumba.





Mwendelezo wa warembo wakiwa tayari kusubiri kuchaguliwa


IONGOZI mwandamizi wa Kianglikana wa Swaziland, Askofu Meshack Mabuza, amemtaka Mfalme Mswati III kuachia madaraka ya kisiasa ili kutoa nafasi Serikali ya kidemokrasia nchini humo.
Askofu Mabuza ameiambia BBC mfumo wa Serikali wa “mambo ya kale” unaofuatwa sasa umeiingiza nchi katika mgogoro mzito wa fedha na uchumi.
Taarifa zinasema Serikali imekiri kuwa mishahara ya wafanyakazi wa Serikali itacheleweshwa mwezi huu kutokana na upungufu wa fedha.


Mfalme Mswati III akikagua gwaride




Mfalme Mswati, mwenye wake 13, ni kiongozi pekee ambaye hushilikia mamlaka yote Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kiongozi huyo amekuwa akishutumiwa kwa kiasi kikubwa kuhusishwa na ufisadi, lakini akaahirisha sherehe zake za kufikisha miaka 25 madarakani mwaka huu kutokana na msukosuko wa fedha nchini humo.
Mpaka sasa Swaziland imekataa kupokea mkopo wa dola za kimarekani milioni 355 kutoka Afrika kusini kuisaidia kulipa gharama mbalimbali, baada ya Pretoria kuitaka nchi hiyo kufanya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi.
‘Visababu’Askofu Mabuza, askofu wa Kianglikana wa Swaziland, aliiambia BBC kuwa matatizo ya Swaziland hayatokwisha iwapo uongozi huo utaendelea kuwepo madarakani.
Alisema, “Jawabu kwa hakika litatokana na mabadiliko ya uongozi wa serikali ya kiutamaduni, kikabaila, na mambo ya kale.” “Lazima ibadilishwe na uongozi wa kidemokrasia wa vyama vingi.”


Mwendelezo wa warembo wakiwa tayari kusubiri kuchaguliwa






Taarifa ya serikali iliyoonekana kabla ya kutolewa rasmi- iliyotiwa saini na mhasibu anayekaimu, AF Mabila- ilisema malipo ya mishahara ya wafanyakazi wa serikali ya Novemba imesogezwa hadi Desemba.
Msemaji wa serikali Percy Simelane aliiambia BBC baraza la mawaziri limekuwa likijadili suala hilo tangu Jumamosi, lakini mpaka sasa hamna muafaka wowote uliofikiwa.
Serikali imesema mgogoro wake wa fedha umesababishwa na msukosuko wa uchumi duniani na kuporomoka kwa mapato ya uongozi huo kutoka umoja wa ushuru wa forodha wa kusini mwa Afrika (sacu), kufuatia makubaliano mapya ya ushuru wa forodha mwingi. Lakini askofu Mabuza, anayetarajiwa kuachia madaraka mwezi ujao, alisema hivyo ni “visababu”.
Alisema, ” Matatizo ya kiuchumi yalikuwepo hata kabla ya kuporomoka kwa uchumi wa dunia kwasababu imekuwa kama hakuna ukuaji wa kiuchumi.”
“Nchi hii imefika hatua ya kuporomoka kabisa.”
Kumekuwa pia na wasiwasi kuwa hospitali za taifa zinaweza kuishiwa na dawa za kufubaza ukimwi ARVs kutokana na upungufu wa fedha. Swaziland, yenye jumla ya watu milioni 1.2, ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya walioathirika na ukimwi duniani.
Takriban watu 230,000 wanaishi na virusi vya ukimwi, ambapo 65,000 wanategemea hospitali za taifa kuwapa dawa hizo za ARV. Vyama vya kisiasa vinazuiwa Swaziland, ambapo Mfalme Mswati amekuwa madarakani tangu mwaka 1986. Wakosoaji wanaishutumu familia hiyo ya kifalme kwa kuwa na matumizi makubwa kupita kiasi, licha ya idadi kubwa ya watu wake wakiishi maisha ya kimaskini.
Msukosuko wa kiuchumi umechochea maandamano dhidi ya uongozi wa mfalme Mswati, lakini wachambuzi wamesema ufalme huo bado unapewa heshima kubwa na Waswaziliand wengi wanaothamini mila na desturi zao.

NAPE ALIVYOWASHA MOTO MBEYA

Sunday 17 July 2011

Wabunge wa  CCM wa mkoa wa Mbeya na kwengineko wakimuongoza Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauyem kuingia uwanja wa Rwandanzovwe mjini Mbeya kwenye mkutano mkubwa wa hadhara



 Katibu wa Vijana na Jimbo la Mbozi wa Chadema Warren Kaminyonga akionyesha kadi yake ya CHADEMA kabla ya kumkabidhi NAPE
 Nape akimkaribisha  Mwenyekiti wa Mtandao wa Chadema wa wanataaluma Prince  Mwaihoja
 Nape akihutubia maelfu ya watu katika uwanja wa Rwandanzovye mjini Mbeya
 Mh. Samwel Sitta akihutubia katika mkutano huo
 Nape akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Rwandanzovwe mjini Mbeya 
 Mjumbe wa NEC, Oganaizesheni Asha Abdallah Juma akihutubia
 Mbunge wa Simanjiro Mh.  Ole Sendeka akihutubia
 Mwenyekiti wa Wabunge wa mkoa wa Mbeya, Prof Mwakyusa akizungumza. Kushoto ni Nape
 Maelefu ya watu  kwenye uwanja wa Rwandanzovwe mjini Mbeya
 Mbunge wa Kyela Dkt. Harrison Mwakyembe akihutubia kwenye mkutano huo
 Nape akicharaza gita wakati wa mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Rwanda, Nzovwe, mjini Mbeya
 Wabunge wa mkoa wa Mbeya, Sitta na Nyarandu wakimuongoza Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kuingia uwanja wa Rwandanzovwe mjini Mbeya kwenye mkutano wa hadhara
Msafara wa pikipiki ukipokea msafara

Hali ya Umeme nchini kuzorota. Mtera kukauka?

 waandishi wa habari wakiwa katika ziara ya Mtera wakipata mawelezo ya awali



ni  Mhandisi  Mkuu wa  Uendeshaji kutoka  kituo cha kuzalisha umeme kwenye bwawa la Mtera, Julius Chomolla  akitoa maelezo kuhusu kipimo cha  kuonyesha  maji  yamejaa  katika  eneo  hilo. Katika kiuto hicho kiwango cha juu cha kuzalisha umeme ni mita 698 wakati cha chini cha kuzalisha nishati hiyo ni mita 690 na jana (juzi) kipimo hicho kilionyesha  mita 690.74, ambapo. Bwawa hilo linazalisha umeme MW 33 badala ya MW 80.



Mhandisi Mkuu wa Uendeshaji kutoka kituo cha kuzalisha umeme kwenye bwawa la Mtera ,Julius Chomolla akionyesha kipimo cha kuonyesha maji yaliyopungua.
 Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiangalia jinsi bwawa la Mtera ilivyopungua maji
 Wanahabari wakitembelea bwawa la Mtera
waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari wakipata maelezo ya uzalishaji wa umeme katika kituo cha Mtera.

BWAWA LA MTERA HALITOSIMAMISHWA KUZALISHA UMEME JAPO KINA CHA MAJI KIPO CHINI KABISA
Picha na Habari na
Magreth Kinabo - MAELEZO


IMEELEZWA kuwa bwawa la Mtera halitosimamishwa kuzalisha umeme kutokana na kupungua kwa kina cha maji kilichosababishwa na ukosefu wa mvu za kutosha.


kauli hiyo ilitolewa jana na Mhandisi Mkuu wa Uendeshaji wa kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera ,Julius Chomolla wakati akizungumza na waandishi wa habari jana(juzi).


" Utaratibu unafanyika wa kuzalisha umeme kwa masaa katika bwawa hili ili uzalishaji usisimame kama ilivyotokea mwaka 2006. hivyo tutaendelea kuzalisha umeme bila ya kusimama hadi tutakapofiklia msimu ujao wa mvua," alisema Chomolla.


Chomolla aloiongeza kuwa kiwango cha umemekinachozalishwa kwa sasa hadi jana(juzi) katika bwawa hilo ni MW 33 badala ya MW80 .


Aliongeza kuwa kiwango cha juu toka usawa wa bahari cha kuzalisha umeme ni mita 698.50 na cha chini mita 690, ambapo siku ya jana(juzi) kilikuwa mita 690.74.


kituo hicho KINAtegemea maji kuto mito miwili ambayo ni Ruaha Mkubwa na Ruaha na Mdogo na Kisigo wakati wa kipindi cha masika.


Kwa mujibu wa Meneja wa Mawasiliano wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) ,Badra Masoud Vituo vbingine vinvyozalisha umeme ni Kihansi kwa sasa ni MW 90 badala ya MW 180,Kidatu MW 40 badala ya 204, New Pangani MW 20 badala ya MW168 na Nyumba ya Mungu ni MW3.5 badala ya MW 8.

ROASTAM AZIZ AJIUZULU NAFASI ZOTE SERIKALINI NA SIASA

Wednesday 13 July 2011


Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, ambaye pia ni mfanyabiashara mkubwa nchini Tanzania, Rostam Aziz, ameachia ngazi leo! Akiongea na wapiga kura wake jimboni kwake Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora, Rostam alitamka kuwa ameamua kuachana na SIASA UCHWARA ili apate muda wa kufanyabiashara zake. Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wanahabari, ametangaza kuachia ngaza nafasi yake ya ubunge wa Igunga na ile ya ujumbe wa NEC! Hii ina maana kwamba Rostam ameamua kujivua gamba mwenywe kabla ya kuvuliwa na kwamba jimbo la Igunga sasa liko wazi!

HOTUBA YA MHE. ROSTAM AZIZ KWA WAZEE WA IGUNGA - TABORA
UTANGULIZI
WAZEE wangu, kwanza kabisa kabla ya kueleza kile ambacho kimenisukuma kuzungumza nanyi leo,

WALISIKIKA WAKISEMA YANGA YA TANZANIA LAKINI SIMBA YA DAR ES SALAAM...

Sunday 10 July 2011


Timu za Simba na Yanga,  leo zimetoana jasho vikali katika fainali ya Kombe la Kagame, uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ubingwa baada ya kuifunga Simba kwa bao 1-0. PICHANI JUU Sehemu ya mashabiki wa Simba wakiishangilia timu yao kabla ya kufungwa. Inayofuata ni mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi (kulia) akiumiliki mpira mbele ya beki wa Yanga, Godfrey Taita.
Beki wa Simba, Kelvin Yondani (kulia) akimzuia mshambuliaji wa Yanga, Davies Mwape.
Wafanyakazi wa Kikosi cha Msalaba Mwekundu, wakimtoa nje ya uwanja mchezaji wa Simba, Mwinyi Kazimoto, baada ya kuumia.
Winga wa Simba akipiga mpira golini mwa Yanga, baada ya kumtoka beki wa timu hiyo, Godfrey Taita (kushoto).
ashabiki wa Simba wakiishangilia timu yao kabla ya kupigwa bao
Kamanda Mkuu wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, David Misime (katikati) leo aliongoza shughuli za usalama uwanjani hapo. Aliokaa nao ni maofisa wenzake.
Mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi, (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa Yanga, Oscar Joshua.

AZAA MAPACHA WATANO UINGEREZA, AAMBIWA ARUDI KWAO NIGERIA

PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS
Bimbo akiwa na mapacha wake sita nchini Uingereza.


....Kabla hajajifungua.
MWANAMKE mmoja raia wa Nigeria, alipotambua ana ujauzito, aliamua kwenda Uingereza akitegemea watoto wange wangepata uraia wa nchi hiyo.


Hata hivyo, baada ya kujifungulia huko, mamlaka za Uingereza zimepinga kutoa uraia kwa watoto hao, licha ya kuwa alifaidika kwa kuhudumiwa akiwa hospitali na mfuko wa bima ya afya.


Mamlaka zilisema kwamba watoto wa mwanamke huyo, aitwaye Bimbo Ayelabola, (33), hawana haki ya moja kwa moja kuwa raia wa Uingereza, licha ya kuzaliwa nchini humo.


Kwa mujibu wa utaratibu huo, mamlala zilisema ili kupata sifa hiyo, mmoja wa wazazi wa watoto hao angekuwa raia wa Uingereza.


Muda wake wa kuishi Uingereza umemalizika Juni 27 mwaka huu na kwamba anaweza kuongezewa muda wa miezi mingine sita ya kuishi humo. Hata hivyo, Bimbo ameamua kulifikisha suala hilo mahakamani akisema uamuzi wowote wa kuwazuia watoto wake kupata uraia utakiuka Sheria ya Uraia wa Uingereza iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009.


Wakili wake alifafanua kuwa kipengelea cha sheria hiyo kinawalinda watu na kuwaruhusu kupata uraia kwa misingi ya kiafya.


Bimbo alikuwa akimeza dawa za kuongeza nguvu alipokuwa nyumbani kwao Lagos, Nigeria, kabla ya kuamua kwenda Uingereza ambapo alipatiwa huduma ya bima ya afya ya dharura akitegemea kujifungua watoto wanne.


Baada ya kujifungua watoto wanne, madaktari waligundua alikuwa na mtoto mwingine wa tano.


Mwanamke huyo ametuma maombi Wizara ya Mambo ya Ndani aongezewe muda wa kuishi Uingereza kwani afya za watoto wake hazijaimarika.


Mapacha wa Bimbo ni Yaseed na Samir, ambapo wa lkike ni Aqeelah, Binish na Zara ambao anasema hawawezi kupata msaada wa kuwalea kutoka kwa ndugu na marafiki zake ambao wengi wapo Uingereza.


Mumewe aitwaye Obi (37), alikwenda Uingereza kumwona akiwa hospitali na alipogundua ana ujauzito wa mapacha, alirejea Nigereia.


Wizara ya Mambo ya Ndani inasubiriwa kuona kama itamwongeza muda mama huyo, na inasemekana inatarajia kumpelekea ankara za huduma alizopewa mwanamke huyo hospitali.


Bimbo amesema hana uwezo wa kulipia ankara hizo na sasa anasaidiwa na Stella (26) rafiki yake waliyekuwa naye tangu shuleni ambapo kila mtoto anahitaji huduma za Pauni 70 kila wiki.


.....Akifikiria mustakabali wake baada ya kuambiwa atarejea kwao Nigeria.

Yanga kumenyana na Simba TAIFA baada ya kutinga fainali CECAFA Cup

Friday 8 July 2011

 Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia ushindi walioupata leo wa magoli 5-4 yaliyopatikana kwa mikwaju ya penati.Yanga imetinga fainali ya mashindano ya Kagame-Castle Cup kwa kuitungua timu ya St. George ya Ethiopia kwa idadi hiyo ya magoli.hivyo Yanga itakutana na Simba katika fainali hiyo itakayochezwa siku ya jumapili ya julai 10 katika uwanja wa Taifa jijini Dar.
 Mashabiki wa timu ya Yanga wakiwa ni wenye furaha sana kwa timu yao kupata ushindi huo na kufanikiwa kutinga fainali ambapo timu yao itakutana na watani wao wa jadi Simba hapo jumapili ya julai 10.
Beki wa timu ya St. George ya Ethiopia,Alula Girma akijaribu kuondosha hatari iliyokuwa ikielekea langoni mwake na Mshambuliaji wa Yanga Jerryson Tegete.
Nurdin Bakari akichuana na beki wa St. Georges.

Wachezaji wa timu ya St. George wakizuiliwa na kina Ras Makunja wakati walipokuwa wakitaka kupiga sebene na  waamuzi wa mchezo kwa madai ya upendeleo.

Baadhi ya Mashabiki wa timu ya Simba wakiwabeza Mashabiki wa timu ya Yanga kwa ujumbe huu.
Dakika tisini za mchezo zimemalizika na haya ndio matokea yalivyo,na hivi sasa dakika thelathini zimeongezwa na mchezo bado unaendelea.
Ndani ya dakika 45 za kipindi cha pili lilitokea zengwe mara baada ya shuti kali lililopigwa na Shadrack Nsajigwa wa Yanga kuingia wavuni lakini kwa mpira uliokuwa umeishatika.hivyo mtafaruku kidogo ulitokea na hatimae muamuzi akasawazisha na mpira ukaendelea kama kawaida.
Sehemu ya Nyavu ilitoboka kutokana na shuti la Nsajigwa ikiwekwa sawa.

SIMBA ILIVYOTINGA FAINALI KAGAME CUP

Beki wa Simba Amir Maftar(kulia), akiondosha mpira langoni mwake huku akizongwa na beki wa El Mereikh, Badrr Eldin Eldod.


Wachezaji wa El Mereikh wakishangilia goli lao la kwanza sambamba na wapenzi wa Yanga walioko jukwaani.


TIMU ya Simba ya jana iliingia fainali ya Kombe la Kagame kwa kuitoa El Mereikh ya Sudan katika mchezo wa kukata na shoka uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo dakika tisini zilimalizika kwa sare ya bao 1-1. Ziliongezwa dakika 30 lakini hakuweza kupatikana mbabe, ndipo ikabidi yapigwe matuta (penalti) ambapo Simba waliibuka washindi kwa mabao 5-4.


Ulimboka Mwakingwe, akiwachambua mabeki wa El Mereikh.


Kipa wa El Mereikh, Isam Elhadary, akibinuka na kuuangalia mpira unavyongia golini ukitoka kichwani mwa Ulimboka Mwakingwe (nyuma yake).


Mashabiki wa Simba wakishangilia baada ya Ulimboka kusawazisha bao.