Mashindano ya kula mjini Morogoro

Friday, 8 July 2011

Wazo Ngosingosi ( kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya ( watatu kulia) mara baada ya kuwa mtu wapili kumaliza shindano la kula chakula kilo moja ya wali,wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, za kimkoa zilizofanyika Julai saba mwaka huu eno la Tarafa ya Lupiro, Wilaya ya Ulanga.
Washiriki wa Mashindano ya kula Wali kilo moja kwa muda wakipata maelezo kabla ya mashindano kuanza.
Maongezi ya hapa na pale.
Kipunga kikiwa tayari tayari kwa ajili ya washiriki wa mashindano.
kazi imeanza hapa.

Mchezo wa mashindano ya kula , ulibuniwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, ' Tanganyika' ambapo aliweza kununua mchele wa kutosha na kwa upende wa kitoweo cha nyama ya kuku , kuku walinunuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu.

Washiriki 14 walijitokeza kati ya hao wanawake walikuwa ni wanne , na ulifanyika siku ya kilele cha maadhimisho hayo ya kimkoa Julai saba, mwaka huu eneo la Tarafa ya Lupiro, Wilaya ya Ulanga na kuhudhiriwa na mamia ya wakati wa eneo hilo pamoja na viongozi wa serikali ngazi ya Wilaya na Mkoa .

Mshindi wa kwanza, Sudi Kilamilo alipatiwa sh: 35,000 na ngao , mshindi wa pili Wazo Ngosingosi , alizawadiwa sh: 25,000 na mshindi wa tatu , Omary Manjawa .Picha na John Nditi.

Miaka 57 ya kuzaliwa TANU yafana

Mzee Constantine Osward Millinga akielezea historia ya chama cha TANU wakati wa sherehe za kuzaliwa kwa chama hicho katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar huku Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa CCM Bara Mh. Pius Msekwa wakimsikiliza
Mzee Constantine Osward Millinga (90), mmoja kati ya waasisi watatu kati ya 17 wa TANU walio hai akiongea wakati wa maadhimisho ya kuzaliwa kwa chama hicho cha kwanza cha siasa nchini ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar Julai 7, 2011

WAMACHINGA WAVURUGA AMANI JIJINI MWANZA

Wednesday, 6 July 2011

amanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro (mwenye kofia nyeusi) akielekea eneo la tukio kutoa amri ambayo kwa kiasi ilirejesha amani baada ya vurugu kushamiri.
Leo kuanzia majira ya saa 3:10 asubuhi kumezuka vurugu jijini Mwanza kati ya wafanyabiashara ndogo ndogo al-maarufu kama Wamachinga na Jeshi la Polisi Mwanza kwa wafanyabiashara hao kudai kufukuzwa eneo lao la biashara tofauti na makubaliano, hali iliyosababisha watu kaadhaa kujeruhiwa na wengine watatu kuhofiwa kupoteza maisha.


Magari mawili ya mfanyabiashara maarufu mkoani hapa Mukeshi vunja bei yamechomwa moto na kuteketea, vibanda kadhaa vimevunjwa, Baadhi ya bidhaa zilizopangwa nje zimeibiwa nayo matairi yamechomwa katikati ya njia panda kuingia mtaa wa Makoroboi kuelekea Soko kuu na kiunganishi cha barabara ya Lumumba Mwanza huku baadhi ya wamachinga hao wakirusha maboksi yaliyoshika moto kwenye majengo yaliyo karibu na eneo hilo kwa nia ya kuyachoma moto.
Vibaka wamepora bidhaa na mali zilizokuwa nje ya Nono Super market na kisha kuchoma friji lilokuwa na vinywaji ambavyo walivinywa kabla ya kuliteketeza.
Kusanyiko la shaka-shaka.
Matairi pia yamechomwa mbele ya lango kuu la soko kuu la jijini Mwanza hali iliyopelekea kufungwa kwa soko hilo nazo biashara kusitishwa.


Friji likiteketea kwa moto.

M-Net's BIG BROTHER AMPLIFIED




KAMA inavyoonekana pichani mambo yanazidi kupamba moto ndani ya mjengo na siku zinazidi kuyoyoma, tuzidi kufuatilia ili kujua nani ataibuka kidedea mwisho wa shindano hili.

SIMBA YATINGA NUSU FAINALI CECAFA

PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS
Kocha Mkuu wa Simba, Moses Basena, akimpa maelekezo mchezaji wake Mohamed  Banka.
Kiungo Mshambuliaji wa Simba Haruna Moshi ‘Boban’ (jezi nyeupe) akimtoka beki wa Bunamwaya, Ronald Seku.
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya  Kombe la  Kagame,  Simba au ‘Wekundu wa Msimbazi’  wa jijini Dar es Salaam, jana walifanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuitandika timu ya Bunamwaya ya Uganda magoli 2-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Katika mchezo huo  uliokuwa na ushindani wa hali ya juu, Simba ilikuwa ya kwanza kujipatia bao dakika ya tisa baada ya shuti la Haruna Moshi ‘Boban’ kumbabatiza Ronald Seku na kutinga wavuni.

Umati wa mashabiki wa Simba wakiishangilia kwa nguvu.
Polisi waliokuwa uwanjani wakifuatilia mpambano huo.
Mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassani ‘Mgosi’, akitafuta mbinu za kuwapita walinzi wa timu ya Bunamwaya,  Ayub Kisaliita na Habib Kavuma.

yanga yatinga nusu fainali kombe la kagame kuipiga red sea ya eritrea bao 6-5

 wachezaji wa red Sea wakimzonga Refa kwa madai kuwa anawauma hasa baada ya refa kuwataka Yanga kurudia penati baada ya kukosa - mara mbili

Beki wa Red Sea akiokoa mpira huku Davies Mwape akiukodolea macho
 KIPA WA YANGA AKIOKOA PENAT I YA MWISHO
 askari wakiweka ulinzi kwa waamuzi wa leo

Mashabiki wa Yanga wakifurahia ushindi
 Mshambuliaji wa Yanga, Davies Mwape akitafuta mbinu za kuwatoka walinzi wa Red Sea katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya kombe la kagame kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam. Yanga ilishinda bao 6-5 za matuta baada ya kumaliza dakika 90 bila kwa bila. Katika penati tano-tano timu zote zilikosa penati moja moja kabla ya Yanga kushinda kwa penati yan mwisho iliyopigwa na Nurdin Bakari
Mshambuliaji wa Yanga, Kigi Makasi akimtoka beki wa Red Sea, Yakob Tekie katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya kombe la kagame kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam. Picha kwa hisani ya Michuziblog

yanga na el mereikh zatoka sare 2-2 kombe la kagame castle cup

Sunday, 26 June 2011

MASHABIKI WA YANGA WAKISHANGILIA MOJA KATI YA MAGOLI YALIYOFUNGWA NA TIMU YAO


Mshambuliaji wa Yanga Davies Mwape akiruka daruga la beki wa  El-Mereikh ya Sudan, Nasr Eldin wakati wa mchezo wa Kombe la Kagame Castle uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2.
PICHA YA PAMOJA YA MANAHODHA WA TIMU ZOTE NA WAAMUZI
MASHABIKI WA SIMBA WAKIIPA SAPOTI EL-MEREIKH
KIKOSI CHA YANGA.
  
KIKOSI CHA EL-MEREIKH YA SUDAN.

Shaggy alipotembelea Usukumani

Shaggy akitumbuiza uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza usiku huu
Wanamuziki wa Shaggy wakifanya vitu vyao jukwaani

Nyomi ya Mwanza







Shaggy baada ya kusimikwa ubalozi wa wa Wasukuma huku Bujora mchana



Balozi wa Wasukuma Shaggy kwenye kiti chake cha enzi



Jaji Mark Bomani akimsimika Shaggy ubalozi wa Wasukuma




Balozi wa Wasukuma akishukuru wananchi wa Mwanza kwa heshima hiyo



Wachezaji wa ngoma ya Kisukuma wakikaribisha wageni



Shaggy akitembelea jumba la Makumbusho la Wasukuma Bujora






Shaggy akiwa kazungukwa na wanautamaduni wa Kisukuma.



TASOTA awards 2011 gala dinner

 Emirates Airlines Staff pose after grabbing a number of awards including the Best Airline of the Year Award during a Tanzania Society of Travel Agents TASOTA) Awards gala night over the weekend at the Movenpick Hotel in Dar es salaam
 TASOTA Chairman Moustafa Khataw presents Travelport's Key Account Manager Rajab Itambo the Chairman's Appreciation Award
Flamenco Dancers from South Africa


Shambulio la bomu laua 25 nchini Nigeria

Shambulio hilo lilitokea muda wa saa kumi na moja jioni watu wakiwa wanastarehe kwenye baa moja mjini Maiduguri.


Kulingana na duru za kiusalama na watu walioshuhudia, watu wanashukiwa kuwa wafuasi wa kundi la boko haram walifika katika ukumbi huo wa starehe wakiwa wamebebwa kwenye pikipiki, kisha wakarusha mabomu kwenye baa hiyo.
KIKUNDI CHA LOCAL ISLAMIC BOKO KINACHOTUHUMIWA


Inasemekana kuwa walirusha mabomu matatu kwenye klabu hicho cha pombe. Milipuko iliotokea imesababisha vifo vya watu 25 na wengine wengi kujeruhiwa.
WANACHAMA WA KIKUNDI CHA BOKO ISLAMIC WAKIWA WAMELAA CHINI


Kufikia usiku wa manane, wafanyikazi wa idara ya huduma za dharura na wazima moto bado walikuwa kwenye eneo la tukio katika harakati za kuokoa majeruhi na kukabiliana na moto.


Ingawa kundi la boko haram halijakiri kutekeleza shambulio hilo, polisi wanahisi kuwa huenda limehusika.


Kundi hilo lenye itikadi kali za dini ya kiisalmu linalopinga elimu ya kisasa, limekuwa likitekeleza mashambulio ya bomu kaskazini mwa Nigeria, ambako pia ni ngome yake.


Boko haram walikiri kuhusika na shambulio la bomu kwenye makao makuu ya polisi mjini Abuja wiki mbili zilizopita.


Tangu kiongozi wa kundi hilo Mohammed Yusuf afe akiwa chini ya ulinzi wa polisi mwaka wa 2009, Kundi hilo lilitangaza vita dhidi ya kikosi hicho na limekuwa likawashambulia kaskazini mwa Nigeria.


Nia ya boko haram ni kuwa sheria za kiislamu zitumike kote nchini Nigeria.


Wafuasi wake pia wamekuwa wakishambulia viongozi wa kitamaduni na maimamu wenye misimamo ya wastani.


Rais Goodluck Jonathan anataka serikali ifanye mazungumzo na kundi hilo ambalo sasa linatishia kuwa changamoto kubwa kwa utawala wake kando na wapiganaji walioko kwenye jimbo la Niger Delta kunapozalishwa mafuta.


Hata hivyo wadadisi wa masuala ya kiusalama wanasema mazungumzo na kundi hilo yatakuwa magumu kuanzisha kwani, uongozi wa Boko haram hauna mfumo wa kuaminika na kwa sasa haijulikani nani ndiye amiri.