MASHABIKI WAWAPIGA SIMBA SC..

Sunday, 19 June 2011

JITIHADI za kikosi cha Simba kutaka kusonga mbele na kuweka rekodi kwenye michuano ya Afrika zilikwama jana baada ya kufungwa mabao 2-0 na DC Motemba ya DR Congo katika mechi ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Michuano ya Kombe la Shirikisho.


Pamoja na hivyo, mechi hiyo ilitawaliwa na vurugu kubwa huku mashabiki wakitumia muda mwingi kurusha chumba na mawe uwanjani hali iliyofanya mkuu wa msafara, Muhsin Balhabou ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya TFF kuwasilisha malalamiko yake kwa kamisaa wa mchezo huo.


Vurugu hizo za watu wa DC Motema Pembe ambayo ililala kwa bao 1-0 jijini Dar es Salaam zilianza mapema hata kabla ya kuanza kwa mechi baada ya kumvua nguo mwandishi Asha Kigundula wa gazeti la Jambo Leo kwa madai ya kumkagua kama ana hirizi.


Viongozi wa Motema Pembe walimvua Asha nguo wakati akienda chooni. Kwa kushirikiana na askari polisi walimshinikiza kufanya hivyo wakati wote ni wanaume, kitu ambacho kamisaa amekubali kuwa ataripoti kwa Caf.


“Kweli wamenivua nguo, wamenidhalilisha na hawajanikuta na chochote. Viongozi wa Simba na TFF wanalishughulikia suala hilo,” alisema Asha.


Vurugu zilizidi kuwa kubwa baada ya mechi kwisha kwa mashabiki kuvamia uwanjani hapo na kulazimisha maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini DR Congo kuingilia kati na kuwahifadhi wachezaji wa Simba uwanjani hapo kwa zaidi ya saa moja.


“Tunalazimika kubaki ndani ya uwanja, hali ni mbaya. Vurugu ni kubwa na watu hawa wanataka kutuua. Kama tungeshinda nakuambia tungekufa, sijaona watu wasiyo wastaarabu kama hawa.


Askari wanawaangalia tu, kweli Congo hakuna serikali. Wametutupia mawe, chupa tokea mechi inaanza,” alisema Balhabou, kiongozi wa msafara.


Aliongeza: “Kamisaa ameona na ameandika kila kitu kwa kuwa tangu mwanzo wa mechi walikuwa wakiturushia mawe uwanjani.”


Matokeo hayo ya jana yameitoa Simba kwenye michuano hiyo kwa jumla ya mabao 2-1 na kufanya izikose Sh milioni 250 kama ingevuka hadi hatua ya makundi.


Katika mchezo huo, Simba ilijitahidi kulinda lango katika dakika za mwanzo lakini kadiri muda ulivyokuwa ukisonga mbele ndivyo ilivyokuwa ikipwaya katika safu ya ulinzi hadi iliporuhusu bao katika dakika ya 38 lililofungwa kwa kichwa na Bokota Labama.


Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, lakini walikuwa Motema Pembe waliopata bao la pili dakika ya 66, kupitia Tresor Salakyaku. Bao hilo lilitokana na uzembe wa mabeki wa Simba walioshindwa kuondosha mpira haraka katika eneo lao la hatari.


Pamoja na Simba kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wao kusawazisha mabao hayo, safu ya ulinzi ya Motema Pembe ilikuwa imara kuhakikisha hairuhusu madhara yoyote langoni kwake na kufanya matokeo hayo kudumu hadi mwisho wa mchezo.

BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA

Mhe.  Waziri Mkuu Peter Mizengo Pinda,
Tunaomba kuanza  kwa kukupa pole kwa majukumu mazito uliyo nayo katika ujenzi wa taifa letu. Pia tunakupongeza kwa uimara na ushupavu wako katika kusimamia masuala mbalimbali ya kimaendeleo nchini.
Mh. Mizengo Pinda
Mhe. Waziri Mkuu,sisi wanafunzi wa kitanzania katika Chuo Kikuu Cha Urafiki – Lumumba kilichopo jijini Moscow inchini Urusi tunaishukuru sana Serikali yetu kwa kuweza kutupatia udhamini wa masomo ya elimu ya juu kupitia Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. Kwani fursa hiyo ni moja ya njia za kuelimisha taifa  na pia kuongeza idadi ya watendaji bora katika sekta mbalimbali nchini.

Mhe. Waziri Mkuu, lengo kuu la waraka huu kwako ni kukufikishia malalamiko yetu moja kwa moja  juu ya kero mbalimbali tunazozipata kuhusiana na zoezi zima la mikopo hii tunayopatiwa na serikali yetu. Tumeamua kufikisha malalamiko haya kwako kwa sababu wahusika wakuu (WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI pamoja na BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU) hawataki kusikiliza kilio chetu. Tumeawaandikia barua nyingi sana kuhusiana na malalamiko yetu pasipo kujibiwa jibu lolote, na sisi hatuwezi kuendelea kukaa kimya huku tukizidi kuumia, wakati serikali ina kila sababu ya kutusikiliza kwani hii ni haki yetu ya msingi kabisa.

Mhe. Waziri Mkuu, malalamiko yetu ni haya yafuatayo:

1:UTARATIBU MBOVU WA MALIPO YA FEDHA ZA ADA.
Kila mwaka bodi imekuwa na utaratibu wa kutokulipa ada kamili za wanafunzi kwa wakati. Baadhi ya wanafunzi hufikia hatua ya kutoa fedha zao za kijikimu ili kufidia mapungufu hayo katika malipo ya ada.
Mfano:
Mwaka 2008/2009 baadhi ya wanafunzi walilazimika kulipa sehemu ya ada toka katika fedha zao za kujikimu. Na pia mpaka leo haijulikani sehemu ile ya ada za wanafunzi hao ilikwenda wapi licha ya kuuliza mara kwa mara juu ya suala hilo Wizarani na Bodi kwenyewe.
Mwaka huu 2010/2011, bodi imechelewa kutulipia ada kwa takrirban miezi 9 (kwani ada ilitakuwa kulipwa mwezi wa 9 mwaka jana(2010) lakini imekuja kulipwa mwaka huu wa 2011 mwezi wa 5, wakati ndiyo mhula wa pili unaisha. Na cha kusikitisha zaidi wanafunzi walio wengi wamelipiwa ada pungufu kwa zaidi ya dola 1000 kwa kila mwanafunzi, na wengine hawakulipiwa kabisa.
Mhe. Waziri Mkuu, hii ni kero kubwa sana kwani mara kwa mara tumekuwa tukifukuzwa madarasani kwa sababu hatujalipa ada. Tunadharirika sana. Na hata sasa baadhi yetu wametangaziwa kutokufanya mitihani yao ya kuhitimu shahada ya kwanza(degree) na wengine mitihani yao ya kufunga mwaka. Na hali hii hutokea kila mwaka.

2:MAKATO KATIKA FEDHA ZA KUJIKIMU
Mhe. Waziri Mkuu, tunasikitika sana kusema kuwa ni jambo lililozoeleka sasa kwa Bodi kutukata fedha zetu za kujikimu kila mwaka . na kila mara tunapodai kiasi kilichokatwa, wamekuwa wakisema fedha zinapungua kwa sababu ya rate of exchange pale wanapobadili fedha za kitanzania (shilingi) kwenda dola za kimarekani (USD), lakini cha ajabu ni kwamba wakati mwingine ada inapopungua bodi huwa inafidia kiasi kilichopungua. Je, ina maana fedha zetu za kujikimu tu ndizo zinazostahili kuathiriwa na rate of exchange na kutokufidiwa kiasi kinachopelea kila mwaka?

Mfano mzuri ni mwaka huu wa 2010/2011. Bodi imetuma kwa kila mwanafunzi fedha pungufu za kujikimu kwa wastani wa dola za kimarekani 477 na bado wakatueleza eti ni kwa sababu ya rate of exchange. Tumewaomba sana watutumie fedha hizo kwani sisi tunaathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na makato hayo, lakini mpaka leo hatujapatiwa jibu lolote wala hatuoni dalili zozote za suala letu hilo kushughulikiwa na Bodi ya mikopo wala Wizara ya elimu.

3:KUTOKUTUMIWA FEDHA ZA BIMA YA AFYA .
Mhe. Waziri Mkuu, mwaka huu wa 2010/2011, serikali haikutupatia kabisa fedha za kulipia bima ya afya. Kwa masharti ya chuoni na Nchini urusi, mwanafunzi kama HUJALIPIA BIMA YA AFYA HUWEZI KUPATIWA HUDUMA YOYOTE ILE YA AFYA, HUWEZI KURUHUSIWA KUFANYA USAJILI WALA KUPATWA VIZA(kila mwaka huwa tunahitajika kuomba viza mpya  na kufanya usajili ili tuweze kuruhusiwa kuendelea na masomo kwa mwaka unaofuata). Licha ya kuikumbusha wizara na bodi juu ya kutupatia fedha hizo, lakini mpaka leo mwaka unaelekea kuisha hatujapatiwa fedha hizo wala hakuna jibu la aina yoyote ile.

4:MWAMBATA WA ELIMU.
Mhe. Waziri Mkuu, ni miaka mingi sasa imepita tangu tuanze kuiomba wizara kutuletea mwambata wa elimu nchini urusi. Matatizo yetu mengi yanachelewa sana kupatiwa ufumbuzi na wakati mwingine yanashindikana  kabisa kupatiwa ufumbuzi kwa sababu hatuna mwambata wa elimu nchini urusi. Mara kwa mara tumelazimika kupeleka matatizo yetu kwa maofisa wa ubalozi ambao nao pia wana majukumu yao mengine tofauti tofauti, tunashukuru wamekuwa wakijitahidi kutusaidia. Lakini kukosekana kwa Mwambata wa elimu bado ni tatizo kubwa sana linalotuathiri wanafunzi nchini urusi.

5: OMBI LA NYONGEZA KATIKA FEDHA ZA KUJIKIMU.
Mhe. Waziri Mkuu, mara kwa mara tumekuwa tukiilalamikia na kuiomba Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi stadi kutupatia nyongeza ya fedha za kujikimu pasipo mafanikio yoyote. Mji tunaoishi (MOSCOW) ni mojawapo ya miji ghali sana duniani, maisha yetu huku yameendelea kuwa duni sana na wakati mwingine tunashindwa hata kupata baadhi ya huduma muhimu. Mara kwa mara tumeijulisha wizara ya elimu, na hata tumeweza kuipatia michanganuo inayoonesha jinsi fedha wanazotupatia kwa sasa zinaishia katika kulipia mambo mbalimbali ya lazima na wakati mwingine tunabakiwa na kiasi kidogo sana cha pesa ambacho ndicho tunalazimika kukitumia kwaajili ya chakula(japokuwa wengi wetu tunakula aidha mlo moja au miwili tu  kwa siku). Kwa kweli tunaiomba serikali kutufikiria katika jambo hili kwani hali tuliyonayo kwa sasa ni mbaya sana, pia ikizingatiwa kuwa nchini Urusi KILA MWAKA MWEZI WA 9 BEI ZA BIDHAA NA GHARAMA ZA HUDUMA MBALIMBALI HUPANDISHWA na hivyo kuzidi kutuathiri zaidi sisi wanafunzi wa kigeni.

Mhe. Waziri Mkuu, tunatumaini kuwa malalamiko, vilio na maombi yetu, utayapokea na kuyafanyia kazi mapema. Tunakutakia afya tele na mafanikio mema katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa taifa letu.

Asante sana.

WANAFUNZI WA KITANZANIA - CHUO KIKUU CHA URAFIKI LUMUMBA, MOSCOW-URUSI.

simba sc Yaonja joto ya jiwe Nigeria nao vijana U-23 wakanyagwa DRC

Timu ya Vijana stars Tanzania U-23 imepigwa 3-0 Huko DRC 3-0 wakati simba imechezewa kandanda safi na kupigwa 3-0 nayo kutupwanje ya mashindano hayo.

Gaddafi asema anataka uchaguzi huru na wa haki

Colonel Muammar Gaddafi
Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amesema ataridhia ufanyike uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utakaosimamiwa na jumuiya ya kimataifa kwa masharti ya kutokuwepo kwa wizi wa kura.
Kauli hiyo iliyotolewa na mtoto wa kiongozi huyo Seif al -Islam imechapishwa katika gazeti la leo la nchini Italia.


Colonel Muammar Gaddafi
Katika mahojiano yake hayo Seif al Islam amesema uchaguzi huo ungeweza kufanyika ndani ya miezi mitatu. Katika makadirio yake ya juu pengine ingekuwa mwishoni mwa mwaka huu, huku akihakikisha uwazi katika ufanikishaji wake.


Amesema unaweza kusimamiwa na taasisi kama Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na hata Jumuiya ya Kujihami ya NATO ambayo imekuwa ikishambulia majeshi ya Gaddafi kwa mabomu.


Mtoto huyo wa Gaddafi alilisitiza kwamba jambo muhimu ni uchaguzi wa wazi, huku akijinasibu kwa kusema hana shaka kwamba umma wa Walibya utamuunga mkono baba yake. Na wanawaona waasi kama waislamu wenye msimamo mkali, magaidi na mamluki.


Kila vita ina wahanga wake
Aidha ameongeza kuwa baba yake atakuwa tayari kukaa chonjo endapo atashindwa uchaguzi lakini kamwe hatokwenda uhamishoni, akisisitiza kwamba amezaliwa Libya, na atazikwa nchini humo.


Mabomu yakirindima Tripol
Hakika mapigano yanaendelea, mpaka sasa inadaiwa waasi wanasonga mbele kuelekea ngome ya Gaddafi, huko mjini Tripoli, wakiwa katika uwanja wa mapigano upande wa magharibi mwa nchi hiyo.


Inaelezwa kwamba wanashikilia vijiji viwili ambavyo wanajeshi wa Gaddafi walikuwa wakivishambulia huku wakifanya jitihada za kusonga mbele zaidi.


Ndege za NATO zikiwa katika operesheni
Makundi mengine ya wapiganaji waasi kwa upande wa Mashariki mwa Libya na mji wa Misrata wanaendelea kukabiliana vikali na wanajeshi wa Gaddafi wenye zana bora za kivita.


Sehemu zilizoteketezwa kabisa na majeshi ya NATO
Kamano mmoja wa waasi, Khalifa Hafter amesema" Kuna maendeleo yameweza kupatikana katika siku tatu zilizopita, hasa upande wa magharibi na pia Misrata kuna mabadiliko, Waasi wanaweza kuamua hatima ya Slitan na kufungua njia ya Tripoli"


Wakati hayo yakiendelea, Umoja wa Afrika umelionya baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba azimio la umoja huo la kuruhusu mashambulizi ya anga nchini Libya litasababisha hatari kubwa.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritania Hamady Ould Hamady amesema pasipo kuitaja moja kwa moja NATO kwamba mashambulizi yanayoendelea ni matakwa ya upande mmoja.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika ya Kusini, Maite Nkoana-Mashabane anaandaa hotuba itakayoituhumu NATO kwa kufanya mashambulizi yanayomlenga Gaddafi. Awali rais wake Jacob Zuma alisema kwamba jumuiya hiyo ya kujihami,operesheni zake zinavuka kikomo cha azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Katika hatua nyingine rais Barack Obama amesisitiza kwamba operesheni za Marekani dhidi ya Libya ni halali, akijibu ukosoaji wa bunge la nchi hiyo kuhusu lengo na uhalali wa ushiriki wa nchi hiyo.


Taarifa ya Ikulu ya Marekani inasema hakukuwepo haja ya kutaka ridhaa ya bunge kwa sababu jukumu la Marekani katika opresheni hiyo ilikuwa ni kuunga mkono tu.


Jitihada za upatanishi zinaendelea ambapo hivi punde ujumbe wa Urusi umewasili nchini Libya kwa ajili ya mazungumzo na serikali ya Muammar Gaddafi.

NAZI UPUNGUZA MAKALI YA UKIMWI

Vyakula vimetufanya tuamini kuwa maradhi mengi hayana tiba. Hiyo inathibitika wazi pale vyakula vinapotoa majibu ya tiba bila sisi wenyewe kujijua. Kwa mfano ni rahisi sana watu kula chakula wakashiba halafu wakawa hai na kusema dawa hii inafaa au dawa ile haifai na kusahau kukitaja chakula kama dawa ya msingi inayobeba mhimili mzima wa tiba zote. Hii ndio sababu madaktari na wauguzi wanakuwa wakali katika kuwasisitiza wagonjwa kula kabla ya kupewa dawa.


Katika ardhi ambayo binadamu hajafanya uharibifu wa mazingira, inaaminika kuwa pamelala tiba za magonjwa yote zikisubiri watu waje wazigundue.


Miaka ya 1980 ugonjwa wa AIDS ulitokea kuua wanaume, wanawake na watoto duniani kote kwa kishindo kikubwa! Watu wengi wamekufa na wengi wataendelea kufa, kitu ambacho ni tishio ulimwenguni kote mpaka hivi sasa. Wakati huo huo vyakula vimeendelea kuwa tiba na mhimili mkubwa kwa afya za waathirika wa magonjwa mbalimbali duniani kote huku gonjwa hili likizidi kuonyesha sura mbaya na ya kutisha zaidi kila kukicha.


Zipo tiba nyingi ambazo binadamu anazipata toka kwenye vyakula anavyokula bila kujua kama anajitibu. Tena kwa bahati nzuri zaidi ni kuwa tiba hizo pia zinapatikana bila gharama yoyote zaidi ya kula chakula, ukitofautisha na gharama za matibabu ya aina nyingine kama hospitali, dawa za kienyeji nk.


Unatakiwa ujue unapokula chakula chochote huwa unajitibu maradhi fulani bila kujijua. Kwa mfano unaweza kujitibu makali ya AIDS Endapo utatumia vyakula hivi vilivyoorodheshwa hapo chini, pamoja na dawa toka hospitali.


Namna ya kufanya:
Utahitaji;
1. Nazi. Yaweza kuwa nazi, mafuta ya nazi, tui la nazi, dafu n.k.
2. Chai mbichi isiyokaushwa.
3. Vyakula - mchanganyiko wa nafaka.


Nazi:
Nazi imewahi kuthibitishwa kuwa na vitu muhimu vinavyoua virusi. Lauric Acid ndiyo acid pekee kwa kuua virusi ambayo inapatikana toka katika nazi na pengine ni toka kwenye maziwa ya mamaake binadamu tu duniani kote.


Je, Ni kweli Nazi inarutubisha afya?
Acid hii ndiyo kitu pekee chenye uwezo wa kuua virusi na ni rahisi kugundua hilo kama utakuwa mtu mwenye kumbukumbu basi nakupa Uthibitisho katika maeneo matatu.
Linganisha afya mbovu za awali za watu waliohamia Dar Es Salaam kama vile wasichana wa kazi za ndani, vijana wanaokuja kusoma au kuutafuta maisha n.k. wakitokea sehemu zisipopatikana nazi. Utamkuta mtu anakuwa hajiamini, haongei sana, mwoga, ngozi yake imejikunja-kunja, miguu imepasuka na pengine hata kitambi cha kwashakoo ni kawaida kwao. Halafu angalia afya zao pale walipokula vyakula vilivyoungwa nazi kwa muda mfupi tu kama miezi mitatu tu wakiwa hapa Dar Es Salaam. Utagundua kuwa afya zao zilibadilika sana.Wananenepa, Mipasuko kwenye miguu inaondoka, Ngozi zinakuwa nyororo, kwashakoo inaondoka, wanakuwa sio waoga tena, wanaongea sana tena kwa kujiamini na kwa kusema yote ni kuwa wanachangamka kiafya.


Kwa wale tuliosoma “Old schools” mtakumbuka tulisoma vitabu vingi vikiwemo Alfu lela Ulela ambavyo vilijumuisha Safari saba za Sindbad Baharia. Katika safari zake aliwahi kutekwa akiwa na wenzie saba baada ya chombo chao kugonga mwamba na kuvunjika. Watekaji waliwafungia ndani na kuwalisha “wali ulioungwa nazi” ili wanenepe kisha wawachinje! Sindbad kwa kujua hilo hakula kiasi kikubwa na baada ya muda mfupi wenzie walinenepa sana na walichinjwa wakaliwa! Yeye alikuwa akikonda siku baada ya siku na kuwafanya maharamia hao kumfungulia atembee tembee awe huru ili aimarike kiafya na ndipo alipopata mwanya wa kutoroka….


Uthibitisho wa mwisho ni pale mtoto mchanga anapofiwa na mama yake basi huwa anaikosa lauric acid toka ziwa la mama na afya yake nadhani wote mmeshuhudia inavyoathirika. Kifupi ni kuwa anatakiwa pamoja na maziwa ya wanyama anayolishwa inatakiwa apate walau kijiko kimoja cha tui la nazi kila siku ili kuilinda afya yake isiporomoke.


Hivyo kama wewe ni muathirika wa maradhi ya aina yoyote, basi tumia dawa za hospitali, halafu ili kuthibitisha hili jaribu kula vyakula vilivyoungwa nazi kwa kiasi kikubwa, au chakula kilichokaangwa kwa mafuta ya nazi, au jenga mazoea ya kutafuna nazi mbichi na pengine ni vizuri zaidi ukaacha tabia ya kunywa soda na kuanza kunywa maji ya madafu pale unaposikia kiu.


Je Nazi yoyote inatibu?
Kama kawaida ya uhusiano wa mmea na udongo ulivyo, zipo nazi ambazo ukizipeleka katika maabara utazikuta zina kiwango kikubwa cha lauric acid au ukakuta lauric acid ipo kidogo au pengine ukakuta nazi haina kabisa lauric acid kwa vile udongo ulipooteshwa nazi kuna kemikali ambazo zinasababisha udongo huo kuwa sio sahihi kuzalisha acid hiyo katika nazi. Kwa kutambua hilo tafiti nyingi zimefanyika na nazi zenye dawa hapa duniani zipo japo chache na zinapatikana kwa kupiga simu no 0768 215 956 au email rotion@live.com Pia mpaka sasa yapo makampuni ya kusindika nazi ambayo yanakamua nazi zenye lauric acid ya kutosha na kuuza kama dawa. Nazi hizo zimeingizwa nchini na ninazitumia kutoa tiba kwa waathirika na hakika zinapunguza idadi ya watu wenye afya mbovu. Lakini mpaka sasa hakuna taarifa zilizowafikia wawekezaji wa ndani hasa katika sekta ya afya ambao ningeweza kushirikiana nao kuitafiti bidhaa hii nchini watu wale na wapone.


Je, Nazi zinapatikana?
Upande wa pili wa shilingi una sura ya nazi kuwa bidhaa ya wenye nazo tu mara baada ya habari hii kuenea. Sasa Vile vile ni vema kwa wizara za kilimo na chakula pamoja na wizara ya afya kukaa chini na kuangalia namna ya kukabiliana na changamoto hii ya kupungua kwa nazi masokoni pamoja na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo ambayo inaweza kufikia shilingi elfu tatu kwa nazi moja endapo theluthi moja tu ya watanzania wataamua kuitumia nazi kama dawa ya kurutubisha afya zao.


Wakati naendelea kukuletea habari hii, ni vema ukaituma email hii kwa watu ishirini au wote katika address book yako ili tupunguze idadi ya watu wenye matatizo ya kiafya. Tusifiche tiba maana kuwa na taifa lenye wagonjwa ni UMASIKINI. Tafadhali tuma sasa.

WATOTO WAPATA CHANJO YA BURE MORO


WATOTO wa chini ya mika mitano leo waliendela kupata chanjo ya magonjwa ya Minyoo na upungufu wa Vitamini A katika mitaa yote ya Mji wa Morogoro.


Mtandao huu ulitembele katika mtaa wa Makaburi A kata ya Mji Mpya na kukuta zoezi hilo likiendelea ambapo watoto wachache walijitokeza kupata chanjo hiyo ya bure.


Wakizungumza na mwandishi wetu manesi waliokutwa katika kituo hicho, Esther Phirimoni [Mwenye gauni la kitenge] na Mwanaidi Ramadhni Lungenga, walidai kwamba zoezi hilo, lililoanza Juni 8 linafika tamati leo mjini humo.

jaji mkuu azindua kampeni ya kuhamasisha utii wa sheria bila kushurutishwa leo

Saturday, 18 June 2011

 JAJI MKUU  MH. MOHAMED CHANDE OTHMAN (SHOTO) AKIZINDUA KAMPENI HIYO JIJINI DAR ES SALAAM LEO MCHANA
 JAJI MKUU MH. MOHAMED CHANDE OTHMAN CHANDE AKIHUTUBIA WAKATI  AKIZINDUA KAMPENI HIYO JIJINI DAR ES SALAAM LEO MCHANA
WADAU MBALIMBALI WAKIFUATILIA UZINDUZI HUO
 IGP-SAID MWEMA AKITOA HOTUBA YAKE
 
ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKISOMA UTENZI
WADAU WALIOSHIRIKI UZINDUZI WA KAMPENI YA JESHI LA POLIS YA UTII WA SHERIA BILA SHURUTI

JAJI Mkuu Mh. Mohamed Chande Othaman amewataka wananchi kutii sheria bila kushurutishwa kwani kufanya hivyo kutavisaidia vyombo vya utoaji haki kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha na ufanisi zaidi.



Aliongeza kuwa kwa kufanya hivyo pia  kutaiwezesha  jamii kuishi kwa amani, usalama na utulivu pamoja na kupunguza hali ya watu kuishi kwa mashaka na wasiwasi, kupunguza matumizi ya nguvu na kuimarika kwa mahusiano ya kiutendaji  kati ya vyombo vya dola na wananchi.


"Kwa jumuiko hili ambalo linashirikisha vyombo na wadau wakuu wa utoaji na usimamizi wa haki, ninathubutu  kusema kuwa kampeni hii nimeipokea kwa moyo mmoja na ninaamini kwamba tutashirikiana kwa chachu ya utekelezaji wa mkakati huu kwa vitendo kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria".


Aidha ametoa wito kwa taasisi za kiserikali na zisizokuwa za kiserikali kujumuika pamoja  katika kampeni hii ya kuhamasisha wananchi kutii sheria bila kushurutishwa.

ROSE MSUYA AWA VODACOM MISS DAR INTER COLLEGE 2011

Miss Dar Inter College 2011,Rose Msuya akiwa katika pozz mara baara ya kunyakua taji hilo usiku huu katika ukumbi wa Sun Cirro,Sinza jijini Dar.
 Miss Dar Inter College,Rose Msuya akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa Pili,Bressiny Ngowi (shoto) na Mshindi wa watatu,Glory Peter.
 Afisa Huduma na Bidhaa wa Vodacom Tanzania,Elihuruma Ngowi akikabidhi zawadi kwa Miss Vodacom Dar Inter College 2011,Rose Msuya kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) usiku huu katika ukumbi wa Sun Cirro,Sinza jijini Dar.
 Tano Bora.
 Washiriki wote jukwaani.

CCM yazitakia heri Vijana U-23 na Simba SC katika michezo yao kesho

Vijana U-23
Simba SC


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezitakia  kila la kheri na kuibuka na ushindi timu za Simba na Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 23  ambazo zinakabiliwa na mechi muhimu Jumamosi hii. 



Wakati  Simba itashuka dimbani na Motema Pembe katika mechi ya marudiano ya  kombe la shirikisho nchini Congo-DRC,  timu ya Vijana ya U-23 itashuka dimbani na vijana wenzao nchini  Nigeria katika mechi muhimu  ya kuwania kufuzu  kucheza fainali za Olimpiki.



Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM) Nape  Nnauye  imesema  kutokana na mechi hizo kuwa muhimu kwa timu hizo na pia kwa Watanzania, yeye binafsi na kwa niaba ya CCM anazitakia kila la heri timu hizo.



“CCM inependa kuona timu hizo zinafanya vizuri na kurejea na ushindi kwa  kuwa itakuwa ni ishara ya Tanzania kuimarisha ki-soka na hivyo kuwa mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kuinua michezo nchini” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

bongofleva fc kukipiga na wanavyuo dodoma kesho jumapili







Timu ya mpira wa miguu (soka) ya Bongofleva Fc inatarajia kushuka dimbani siku ya jumapili mjini Dodoma,ambapo itakwaana vilivyo na kombaini ya Wanavyuo Dodoma katika uwanja wa Jamuhuri.Aidha kwa sasa timu ya Bongofleva FC inajifua katika viwanja vya Lidaz,Kinondoni jijini Dar, kwa mujibu wa kiongozi wa timu hiyo Rich One.

CYNTHIA KIMASHA ATWAA TAJI LA MISS CHANG’OMBE 2011


 Picha ya kwanza juu Miss Chang’ombe 2011, Cynthia Kimasha, akiwapungia mkono mashabiki wake muda mfupi baada ya kutwaa taji hilo. Picha ya pili juu Miss Chang’ombe 2010, ambaye pia ni Miss Tanzania mwaka 2010/2011, Genevieve Emmanuel Mpangala, akiwaaga mashabiki wake kwa kupunga mkono muda mfupi kabla ya kukabidhi taji hilo.
KATIKA kinyang’anyiro cha kumsaka mlimbwende wa kitongoji cha Miss Chang’ombe 2011/12 usiku wa kuamkia leo, Cynthia Kimasha amewabwaga warembo wengine 12 na kulitwaa taji la kitongoji hicho.   Tukio hilo lilifanyika Temeke ndani ya ukumbi wa TCC Club, Changombe jijini Dar es Salaam, likisindikizwa na bendi ya Mapacha Watatu, na mashabiki kibao kutoka pande mbalimbali.

 Genevieve (kulia) akimkabidhi taji Cynthia Kimasha mara baada ya kutangazwa mshindi.


 Cynthia (katikati), akiwa kwenye pozi na mshindi wa pili Husna Twalib (kushoto), na mshindi wa tatu Joyce Mawenda baada ya kuibuka kidedea.


 Baadhi ya mapaparazi na mashabiki wa shindano hilo wakichukua picha za kumbukumbu kwenye kinyang’anyiro hicho.


 Baadhi ya wadhamini wa shindano hilo wakifuatilia mchakato mzima ulivyokuwa.


 Mashabiki waliojitokeza kwenye mchakato huo wakifuatilia kwa furaha tele zoezi hilo.


Mwanamuziki wa Mapacha Watatu, Khaleed Chuma ‘Chokoraa’ (katikati), akiongoza safu ya wanenguaji wake kusherehesha mashindano hayo.

Abiria wa Bajaji ajeruhiwa katika ajali

Baadhi ya madereva wa Bajaj wakiinyoosha Bajaj iliyohusika katika ajali hiyo.


MWANAMKE mmoja amejeruhiwa asubuhi ya leo baada ya pikipiki ya Bajaj namba T492 BHD iliyokuwa imembeba kugonga gari dogo aina ya Carina maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam. Abiria huyo ambaye jina lake halikufahamika, na ambaye alikuwa akiendeshwa na mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja tu la Jonas, alikimbizwa hospitali mara moja na wafuatiliaji wa tukio hilo wanasema hali yake inaendelea vizuri.




Sura halisi ya Bajaj baada ya ajali.




Madereva wa Bajaj wakiamua ugomvi uliofuatia baada ya tukio hilo.




Wapita njia wakilishangaa gari lililohusika katika ajali hiyo.

UTEUZI WA NAIBU GAVANA BENKI KUU YA TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Daktari Natu El-Maamry Mwamba kuwa Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania. Dkt. Mwamba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt Enos Bukuku, ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Katibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwezi April, 2011. Uteuzi huu unaanza tarehe 13 Juni, 2011.
Kabla ya uteuzi huu, Dkt Natu El-Maamry Mwamba, alikuwa mhadhiri mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Uchumi.
Phillemon L. Luhanjo
Katibu Mkuu Kiongozi
Ikulu,
Dar Es Salaam

Press Conference yahairishwa!


Press Conference iliyopangwa kufanyika leo tarehe 17Juni, 2011
katika Ofisi za Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imepangwa
kufanyika kesho tarehe 18 Juni, 2011 saa 4.00 asubuhi wale wote waliotaarifiwa kuhudhuria Press Conference ya Leo mnaombwa kuhudhuria kesho tarehe 18 Juni, 2011saa 4.00 asubuhi.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
Ahsante na kazi njema.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
17 Juni, 2011

Chadema wamshtaki Makinda

KAMBI ya Upinzani Bungeni imemshtaki Spika, Anne Makinda katika Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge, ikimtuhumu kumkingia kifua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda asiwajibishwe na Bunge.Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Spika Makinda kuzuia kujibiwa kwa swali la Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kuhusu sababu za Serikali kutowafikisha mahakamani askari polisi waliohusika katika mauaji ya raia 72 yaliyofanyika katika kipindi cha kati ya mwaka 2008 na mwaka huu.

Mbali ya Lissu, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Esther Matiko naye alitaka kupata maelezo kutoka kwa Waziri Mkuu ya sababu za kutofikishwa mahakamani kwa askari waliohusika na mauaji ya raia katika eneo la Nyamongo, wilayani Tarime.

Wabunge hao walifanya hivyo wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, yanayoulizwa kila Alhamisi wakati Bunge linapokutana.

Spika Makinda alizuia kujibiwa kwa maswali hayo kwa maelezo kuwa masuala hayo yako mahakamani na kwamba kuyajibu kutakuwa ni kuingilia uhuru wa Mahakama ambayo mara kadhaa, imelilalamikia Bunge kuwa limekuwa likiingilia huru wake.

Maelezo hayo yalionekana kutoiridhisha Kambi ya Upinzani ambayo iliamua kumshtaki Spika katika Kamati hiyo ili ichunguze uamuzi wake na baadaye kutoa uamuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Lissu ambaye pia Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Chadema, alisema tayari kambi yake imeshakamilisha maandalizi ya hati ya malalamiko ya wabunge hao na kwamba ingewasilishwa kwa Katibu wa Bunge jana jioni.

“Tusingependa kufanya hayo maana vinginevyo tunaonekana kama tunahoji uwezo wa Mheshimiwa Spika, lakini hatuna jinsi imebidi. Tumempeleka katika Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge kwa sababu kuacha uamuzi potofu wa Spika wa Bunge usimame, itakuwa ni ‘precedent’ (kitangulizi cha jambo) ya hatari kwa Bunge letu kwa sababu uamuzi huo kuachwa bila kupingwa, unaweza kutumiwa katika mijadala mingine katika siku zijazo,” alisema Lissu.

Alisema vitendo hivyo vya Makinda ni vya ukiukwaji wa kanuni za kudumu za Bunge na kwamba katu Kambi ya Upinzani haitakuwa tayari kumwacha aendeshe Bunge kama anavyoona binafsi.

“Spika wa Bunge ana mamlaka makubwa sana kiuamuzi, lakini anatakiwa kufuata kanuni na kanuni kuu muda wote ni ya nane inayomtaka kuendesha shughuli za Bunge na kutoa uamuzi kwa haki, uadilifu na bila chuki wala upendeleo wowote kwa kuongozwa na Katiba, sheria na kanuni,” alisema Lissu ambaye kitaaluma ni mwanasheria.

Lissu alisema Spika Makinda pia anapaswa kufuata uamuzi wa maspika waliomtangulia na kuzingatia uzoefu, mila na desturi za mabunge mengine yanayofuata utaratibu unaofafana na kufuatwa na Bunge la Tanzania.

Mbunge huyo alidai kwamba hiyo si mara ya kwanza kwa Spika Makinda kutoa uamuzi ulioonekana kumkingia kifua Waziri Mkuu wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo.

“Itakumbukwa kwamba wakati wa Mkutano wa Pili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uliofanyika Februari mwaka huu, Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema aliomba mwongozo wa Spika kutokana na kauli ya uongo iliyotolewa na Waziri Mkuu kuhusu mauaji ya Arusha. Baada ya kutoa mwongozo alioombwa, Spika wa Bunge alimkemea Mheshimiwa Lema na kumtaka athibitishe kauli yake juu ya uongo wa Waziri Mkuu,” alisema Lissu.

Alisema hata hivyo, Lema alipotoa uthibitisho wake, Spika Makinda alizima mjadala kwa kukalia uthibitisho wa Lema... “Hadi leo Watanzania hawajaambia chochote juu ya jambo hilo, lakini kuna siku tutakumbushia hilo ili wananchi wajue ukweli.”

Mbunge huyo alidai kwamba uamuzi wa Spika kuhusu swali lake, aliufanya bila kuuliza au kupewa taarifa sahihi kuhusu mauaji ya Tarime na kesi dhidi yake na wenzake.

“Hii ni hatari sana kwa uendeshaji bora wa Bunge, kama Spika ambaye pia ni kiongozi wa Bunge atakuwa anatoa uamuzi ambao hana taarifa sahihi juu yake… hadhi na heshima ya Bunge itashuka kwa sababu wananchi wataona Spika anatoa uamuzi kwa lengo la kuwakingia kifua mawaziri na Serikali ili wasiwajibishwe bungeni. Hii ikitokea ni hatari kwa demokrasia yetu kibunge,” alisema.

Alisema yeye na wenzake saba wanakabiliwa na mashtaka ya kuingia kijinai katika eneo la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime, kufanya mkusanyiko haramu katika eneo hilo na kuwazuia Mganga wa Hospitali ya Wilaya na askari polisi kufanya uchunguzi wa miili ya marehemu waliouawa katika Mgodi wa Nyamongo na kwamba mashtaka hayo si ya mauaji na kwamba haikuwa sahihi kwa Spika kuzuia maswali yake.

Alipoulizwa juu ya imani yake kwa Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Lissu alisema hana sababu za kuamini kwamba pamoja na kuwa ina idadi kubwa ya wabunge wa CCM, itaacha uadilifu wake na kupindisha haki.

Mbunge huyo alisema kwa mujibu wa kanuni, wakati kamati hiyo yenye wajumbe 15 itakapoketi kuchunguza malalamiko hayo, Spika ambaye pia ndiye wake na naibu wake, watapaswa wasikalie kiti hicho na badala yake, wajumbe watamchagua mmoja wao kuendesha kikao cha uchunguzi.

Alipotakiwa kuzungumzia hatua hiyo, Makinda ambaye jana asubuhi hakuendesha Kikao cha Bunge alijibu kwa simu: “Niko kwenye kikao." Alipotafutwa tena, simu yake ilipokelewa na msaidizi wake ambaye alisisitiza kuwa bado alikuwa katika kikao.