Vijana U-23 |
Simba SC |
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezitakia kila la kheri na kuibuka na ushindi timu za Simba na Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 23 ambazo zinakabiliwa na mechi muhimu Jumamosi hii.
Wakati Simba itashuka dimbani na Motema Pembe katika mechi ya marudiano ya kombe la shirikisho nchini Congo-DRC, timu ya Vijana ya U-23 itashuka dimbani na vijana wenzao nchini Nigeria katika mechi muhimu ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Olimpiki.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM) Nape Nnauye imesema kutokana na mechi hizo kuwa muhimu kwa timu hizo na pia kwa Watanzania, yeye binafsi na kwa niaba ya CCM anazitakia kila la heri timu hizo.
“CCM inependa kuona timu hizo zinafanya vizuri na kurejea na ushindi kwa kuwa itakuwa ni ishara ya Tanzania kuimarisha ki-soka na hivyo kuwa mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kuinua michezo nchini” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
0 comments:
Post a Comment