yanga na el mereikh zatoka sare 2-2 kombe la kagame castle cup

Sunday 26 June 2011

MASHABIKI WA YANGA WAKISHANGILIA MOJA KATI YA MAGOLI YALIYOFUNGWA NA TIMU YAO


Mshambuliaji wa Yanga Davies Mwape akiruka daruga la beki wa  El-Mereikh ya Sudan, Nasr Eldin wakati wa mchezo wa Kombe la Kagame Castle uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2.
PICHA YA PAMOJA YA MANAHODHA WA TIMU ZOTE NA WAAMUZI
MASHABIKI WA SIMBA WAKIIPA SAPOTI EL-MEREIKH
KIKOSI CHA YANGA.
  
KIKOSI CHA EL-MEREIKH YA SUDAN.

Shaggy alipotembelea Usukumani

Shaggy akitumbuiza uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza usiku huu
Wanamuziki wa Shaggy wakifanya vitu vyao jukwaani

Nyomi ya Mwanza







Shaggy baada ya kusimikwa ubalozi wa wa Wasukuma huku Bujora mchana



Balozi wa Wasukuma Shaggy kwenye kiti chake cha enzi



Jaji Mark Bomani akimsimika Shaggy ubalozi wa Wasukuma




Balozi wa Wasukuma akishukuru wananchi wa Mwanza kwa heshima hiyo



Wachezaji wa ngoma ya Kisukuma wakikaribisha wageni



Shaggy akitembelea jumba la Makumbusho la Wasukuma Bujora






Shaggy akiwa kazungukwa na wanautamaduni wa Kisukuma.



TASOTA awards 2011 gala dinner

 Emirates Airlines Staff pose after grabbing a number of awards including the Best Airline of the Year Award during a Tanzania Society of Travel Agents TASOTA) Awards gala night over the weekend at the Movenpick Hotel in Dar es salaam
 TASOTA Chairman Moustafa Khataw presents Travelport's Key Account Manager Rajab Itambo the Chairman's Appreciation Award
Flamenco Dancers from South Africa


Shambulio la bomu laua 25 nchini Nigeria

Shambulio hilo lilitokea muda wa saa kumi na moja jioni watu wakiwa wanastarehe kwenye baa moja mjini Maiduguri.


Kulingana na duru za kiusalama na watu walioshuhudia, watu wanashukiwa kuwa wafuasi wa kundi la boko haram walifika katika ukumbi huo wa starehe wakiwa wamebebwa kwenye pikipiki, kisha wakarusha mabomu kwenye baa hiyo.
KIKUNDI CHA LOCAL ISLAMIC BOKO KINACHOTUHUMIWA


Inasemekana kuwa walirusha mabomu matatu kwenye klabu hicho cha pombe. Milipuko iliotokea imesababisha vifo vya watu 25 na wengine wengi kujeruhiwa.
WANACHAMA WA KIKUNDI CHA BOKO ISLAMIC WAKIWA WAMELAA CHINI


Kufikia usiku wa manane, wafanyikazi wa idara ya huduma za dharura na wazima moto bado walikuwa kwenye eneo la tukio katika harakati za kuokoa majeruhi na kukabiliana na moto.


Ingawa kundi la boko haram halijakiri kutekeleza shambulio hilo, polisi wanahisi kuwa huenda limehusika.


Kundi hilo lenye itikadi kali za dini ya kiisalmu linalopinga elimu ya kisasa, limekuwa likitekeleza mashambulio ya bomu kaskazini mwa Nigeria, ambako pia ni ngome yake.


Boko haram walikiri kuhusika na shambulio la bomu kwenye makao makuu ya polisi mjini Abuja wiki mbili zilizopita.


Tangu kiongozi wa kundi hilo Mohammed Yusuf afe akiwa chini ya ulinzi wa polisi mwaka wa 2009, Kundi hilo lilitangaza vita dhidi ya kikosi hicho na limekuwa likawashambulia kaskazini mwa Nigeria.


Nia ya boko haram ni kuwa sheria za kiislamu zitumike kote nchini Nigeria.


Wafuasi wake pia wamekuwa wakishambulia viongozi wa kitamaduni na maimamu wenye misimamo ya wastani.


Rais Goodluck Jonathan anataka serikali ifanye mazungumzo na kundi hilo ambalo sasa linatishia kuwa changamoto kubwa kwa utawala wake kando na wapiganaji walioko kwenye jimbo la Niger Delta kunapozalishwa mafuta.


Hata hivyo wadadisi wa masuala ya kiusalama wanasema mazungumzo na kundi hilo yatakuwa magumu kuanzisha kwani, uongozi wa Boko haram hauna mfumo wa kuaminika na kwa sasa haijulikani nani ndiye amiri.

Wadau Moscow wala ndondo






KWA PICHA ZAIDI GONGA HAPA

Where is Job Security in Tanzania? Jambo Plastics Ltd yafukuza wafanyakazi wake wote

UONGOZI wa Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za plastiki cha Jambo Plastics Ltd kilichopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam kimewatimua kazi wafanyakazi wote wa kiwanda hicho kwa madai ya kuandaa mgomo wa kudai maslahi bora katika kiwanda hicho.


Wafanyakazi hao walipofika kiwandani hapo walikuta matangazo getini kuwa hawahitajiki kiwandani hapo na waondoke wakatafute ajira sehemu nyingine. Baada ya kuona matangazo hayo ambayo hayakuwa na maelezo zaidi, wafanyakazi hao wakajikusanya eneo hilo kupinga agizo hilo.
Wafanyakazi hao wakiwa wamepumzika kando ya Uzio wa kiwanda hicho

Bungeni: Lowassa asema Serikali ina woga

Friday 24 June 2011

MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa ameiambia Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwa inasumbuliwa na ugonjwa wa woga katika kutoa uamuzi magumu na matokeo yake mambo yake mengi hayaendi kama yalivyopangwa.
Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza katika utawala huu wa awamu ya nne, pia akaitaka Serikali hiyo kubadilika.
habari kamili hapa

Tanzania kinara huduma bora Afrika

UMOJA wa Mataifa (UN), umeitangaza Tanzania kuwa mshindi katika utoaji wa huduma bora za utumishi wa umma kwa jamii barani Afrika, katika maadhimisho wa Wiki ya Utumishi wa Umma, yaliyohitimishwa jana.
HABARI KAMILI HAPA

Waziri afuatwa na mkewe bungeni

Dodoma
Mke wa Waziri wa Serikali ya Tanzania anayetumikia wizara nyeti, (jina limehifadhiwa), amemuibukia mumewe bungeni kisa uwepo wa muigizaji Wema Abraham Sepetu aliyekuwa mjini hapa hivi karibuni.
HABARI KAMILI HAPA

Haruna "Fabregas" atua Jangwani

Bajeti yapita, Mbowe arudisha shangingi

Wednesday 22 June 2011


BAJETI ya Serikali ya Tanzania kwa mwaka wa fedha 2011/12, imepita jana.
HABARI KAMILI HAPA
Balozi wa China Nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete

VURUGU kubwa zilizuka juzi kwenye kituo cha Polisi Babati Mjini mkoani Manyara baada ya wafanyakazi wa kampuni inayojenga barabara ya Chico, raia wa China kumpiga mkuu wa kituo hicho, ASP Shaaban Minginye na mkuu wa polisi jamii mkoani humo, ASP Morris Okinda.
HABARI KAMILI HAPA

Mbowe ataka yafanyike mabadiliko ya sera na sheria


Atoa miezi sita mashangingi yauzwe, posho zifutwe
HABARI KAMILI HAPA

CCM yafanya mazungumzo na wapinzani Ujerumani

CCM yafanya mazungumzo na wapinzani UjerumaniKATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye (wapili kushoto), akizungumza na kiongozi kutoka chama cha upinzani cha SPD cha Ujerumani ambacho kinaongoza Jiji la Humberg nchini humo, Wolfgang Schmidt, (wapili kulia), wakati kiongozi huyo na ujumbe wake walipomtembelea na kuwa na mazungumzo naye, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam jana. Wapili kulia ni Stefan Herms kutoka chama hicho