AZAA MAPACHA WATANO UINGEREZA, AAMBIWA ARUDI KWAO NIGERIA

Sunday, 10 July 2011

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS
Bimbo akiwa na mapacha wake sita nchini Uingereza.


....Kabla hajajifungua.
MWANAMKE mmoja raia wa Nigeria, alipotambua ana ujauzito, aliamua kwenda Uingereza akitegemea watoto wange wangepata uraia wa nchi hiyo.


Hata hivyo, baada ya kujifungulia huko, mamlaka za Uingereza zimepinga kutoa uraia kwa watoto hao, licha ya kuwa alifaidika kwa kuhudumiwa akiwa hospitali na mfuko wa bima ya afya.


Mamlaka zilisema kwamba watoto wa mwanamke huyo, aitwaye Bimbo Ayelabola, (33), hawana haki ya moja kwa moja kuwa raia wa Uingereza, licha ya kuzaliwa nchini humo.


Kwa mujibu wa utaratibu huo, mamlala zilisema ili kupata sifa hiyo, mmoja wa wazazi wa watoto hao angekuwa raia wa Uingereza.


Muda wake wa kuishi Uingereza umemalizika Juni 27 mwaka huu na kwamba anaweza kuongezewa muda wa miezi mingine sita ya kuishi humo. Hata hivyo, Bimbo ameamua kulifikisha suala hilo mahakamani akisema uamuzi wowote wa kuwazuia watoto wake kupata uraia utakiuka Sheria ya Uraia wa Uingereza iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009.


Wakili wake alifafanua kuwa kipengelea cha sheria hiyo kinawalinda watu na kuwaruhusu kupata uraia kwa misingi ya kiafya.


Bimbo alikuwa akimeza dawa za kuongeza nguvu alipokuwa nyumbani kwao Lagos, Nigeria, kabla ya kuamua kwenda Uingereza ambapo alipatiwa huduma ya bima ya afya ya dharura akitegemea kujifungua watoto wanne.


Baada ya kujifungua watoto wanne, madaktari waligundua alikuwa na mtoto mwingine wa tano.


Mwanamke huyo ametuma maombi Wizara ya Mambo ya Ndani aongezewe muda wa kuishi Uingereza kwani afya za watoto wake hazijaimarika.


Mapacha wa Bimbo ni Yaseed na Samir, ambapo wa lkike ni Aqeelah, Binish na Zara ambao anasema hawawezi kupata msaada wa kuwalea kutoka kwa ndugu na marafiki zake ambao wengi wapo Uingereza.


Mumewe aitwaye Obi (37), alikwenda Uingereza kumwona akiwa hospitali na alipogundua ana ujauzito wa mapacha, alirejea Nigereia.


Wizara ya Mambo ya Ndani inasubiriwa kuona kama itamwongeza muda mama huyo, na inasemekana inatarajia kumpelekea ankara za huduma alizopewa mwanamke huyo hospitali.


Bimbo amesema hana uwezo wa kulipia ankara hizo na sasa anasaidiwa na Stella (26) rafiki yake waliyekuwa naye tangu shuleni ambapo kila mtoto anahitaji huduma za Pauni 70 kila wiki.


.....Akifikiria mustakabali wake baada ya kuambiwa atarejea kwao Nigeria.

0 comments:

Post a Comment