IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
WACHEZAJI na mashabiki wa Yanga waliokuwapo katika mchezo wa kirafiki ulioikutanisha timu hiyo na kikosi cha Ilala juzi Jumamosi waliamua kujisaidia aja ndogo katika moja ya kuta za Uwanja wa Kaunda kutokana na uhaba wa vyoo.
Championi Jumatatu lilishuhudia idadi kubwa ya wachezaji wa Yanga wakijisaidia katika ukuta wa uwanja huo bila kujali lolote kwani hapakuwa na choo jirani na sehemu hiyo ya kuchezea. Vyoo vipo katika jengo la klabu hiyo mita chache kutoka uwanjani.
Inapotokea mchezaji au shabiki akakumbwa na haja, hatoweza kwenda katika jengo la klabu kujisaidia kutokana na umbali uliopoa pia kupata shida ya kuingia na kutoka katika geti kuu.
Licha ya Yanga kusifika kuwa na uwanja wake binafsi, kitendo cha Uwanja wa Kaunda kukosa choo huku ukitumika kwa mechi za kirafiki za timu hiyo, kinaiondolea sifa klabu hiyo ambayo ni mabingwa wa soka Tanzania Bara.
Akizungumza na gazeti hili uwanjani hapo, Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu alisema umati uliofurika katika mchezo wao dhidi ya Ilala ulioisha kwa suluhu umeipa faraja klabu yake na kupata hamu ya kuutumia uwanja huo kwa mechi zake za kirafiki, kwani kila shabiki alilipa Sh 3000.
Hata hivyo, Sendeu alikiri kuwepo kwa kasoro ndogo ndogo katika uwanja huo.
0 comments:
Post a Comment