Mzee Malecela taabani

Tuesday, 21 June 2011

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Waziri Mkuu Mstaafu, John Samuel Malecela yupo taabani, amefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo.
Spika wa Bunge la Jmhuri ya Muungano wa Tanzania, Anna Makinda aliwatangazia wabunge leo kabla ya kuahirisha kikao cha asubuhi kuwa Malecela ni mgonjwa.
Alisema, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela haonekani bungeni kwa sababu Mzee Malecela ni mgonjwa.
Kilango ni mke wa ndoa wa mzee Malecela.
“Waheshimiwa wabunge kwa siku kadhaa mheshimiwa Anne Kilango haonekani, yupo anamuuguza mzee Malecela kwa sababu amefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo,” alisema spika leo.
Hata hivyo, Spika Makinda hakueleza hali ya Malecela inaendeleaje, kama ana nafuu ama la.

0 comments:

Post a Comment