Timu za Simba na Yanga, leo zimetoana jasho vikali katika fainali ya Kombe la Kagame, uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ubingwa baada ya kuifunga Simba kwa bao 1-0. PICHANI JUU Sehemu ya mashabiki wa Simba wakiishangilia timu yao kabla ya kufungwa. Inayofuata ni mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi (kulia) akiumiliki mpira mbele ya beki wa Yanga, Godfrey Taita.
Beki wa Simba, Kelvin Yondani (kulia) akimzuia mshambuliaji wa Yanga, Davies Mwape.
Wafanyakazi wa Kikosi cha Msalaba Mwekundu, wakimtoa nje ya uwanja mchezaji wa Simba, Mwinyi Kazimoto, baada ya kuumia.
Winga wa Simba akipiga mpira golini mwa Yanga, baada ya kumtoka beki wa timu hiyo, Godfrey Taita (kushoto).
ashabiki wa Simba wakiishangilia timu yao kabla ya kupigwa bao
Kamanda Mkuu wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, David Misime (katikati) leo aliongoza shughuli za usalama uwanjani hapo. Aliokaa nao ni maofisa wenzake.
0 comments:
Post a Comment