SIMBA ILIVYOTINGA FAINALI KAGAME CUP

Friday, 8 July 2011

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Beki wa Simba Amir Maftar(kulia), akiondosha mpira langoni mwake huku akizongwa na beki wa El Mereikh, Badrr Eldin Eldod.


Wachezaji wa El Mereikh wakishangilia goli lao la kwanza sambamba na wapenzi wa Yanga walioko jukwaani.


TIMU ya Simba ya jana iliingia fainali ya Kombe la Kagame kwa kuitoa El Mereikh ya Sudan katika mchezo wa kukata na shoka uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo dakika tisini zilimalizika kwa sare ya bao 1-1. Ziliongezwa dakika 30 lakini hakuweza kupatikana mbabe, ndipo ikabidi yapigwe matuta (penalti) ambapo Simba waliibuka washindi kwa mabao 5-4.


Ulimboka Mwakingwe, akiwachambua mabeki wa El Mereikh.


Kipa wa El Mereikh, Isam Elhadary, akibinuka na kuuangalia mpira unavyongia golini ukitoka kichwani mwa Ulimboka Mwakingwe (nyuma yake).


Mashabiki wa Simba wakishangilia baada ya Ulimboka kusawazisha bao.

0 comments:

Post a Comment