SIMBA YATINGA NUSU FAINALI CECAFA

Wednesday, 6 July 2011

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS
Kocha Mkuu wa Simba, Moses Basena, akimpa maelekezo mchezaji wake Mohamed  Banka.
Kiungo Mshambuliaji wa Simba Haruna Moshi ‘Boban’ (jezi nyeupe) akimtoka beki wa Bunamwaya, Ronald Seku.
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya  Kombe la  Kagame,  Simba au ‘Wekundu wa Msimbazi’  wa jijini Dar es Salaam, jana walifanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuitandika timu ya Bunamwaya ya Uganda magoli 2-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Katika mchezo huo  uliokuwa na ushindani wa hali ya juu, Simba ilikuwa ya kwanza kujipatia bao dakika ya tisa baada ya shuti la Haruna Moshi ‘Boban’ kumbabatiza Ronald Seku na kutinga wavuni.

Umati wa mashabiki wa Simba wakiishangilia kwa nguvu.
Polisi waliokuwa uwanjani wakifuatilia mpambano huo.
Mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassani ‘Mgosi’, akitafuta mbinu za kuwapita walinzi wa timu ya Bunamwaya,  Ayub Kisaliita na Habib Kavuma.

0 comments:

Post a Comment