IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
MGOGORO ndani ya Umoja wa Vijana wa CCCM (UVCCM), mkoani Arusha umevuta kasi baada ya baadhi ya vijana wa umoja huo kutishia kufunga ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa, Mary Chatanda ili kushinikiza uondoke madarakani.
Habari zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kwamba vijana hao walipanga kufunga ofisi hiyo jana, lakini baadaye walibadili uamuzi na kukubaliana kutekeleza azima hiyo wakati katibu huyo wa CCM akiwa bungeni mwezi ujao.
Mwenyekiti wa kamati ya mahusiano ya UVCCM, Ally Bananga alisema jana kuwa msimamo wa vijana ni kutolala mpaka Chatanda aondoke madarakani.
Kauli hiyo ya Bananga, imekuja siku moja baada ya Makamu Mwenyekiti wa moja huo, ngazi ya Taifa, Beno Malisa kudai kuwa anasikitishwa na kauli zilizotolewa na vijana wenzao mkoani Arusha.
Malisa alisema kutokana na hali hiyo atatuma kamati ya maadili ambayo itakutana na makundi yanayolumbana mkoani Arusha.
Bananga alisema ana unga mkono kamati hiyo ya maadili kwenda mkoani Arusha kuzungumza na makundi yote na aliitahadhirisha kamati hiyo kwamba suala la Chatanda kung ‘oka ni lazima.
“Sisi tuko tayari kuipa ushirikiano kamati hiyo ya maadili, lakini suala la Chatanda kuondoka Arusha liko pale pale tunaomba kuiambia tume hiyo kabla haijawasili kabisa,”alisema Bananga.
Alisema endapo kamati hiyo itaonekana kupendelea ili katibu huyo aendelee kushikilia nafasi yake ya ukatibu wa CCM mkoani hapa, kamwe hali ya hewa haitatulia na kwamba Chatanda atangolewa kwa gharama yoyote.
“Sikiliza endapo Chatanda asipong’ooka tutapambana mpaka kieleweke, hapa ni aluta continua na tunaitaka tume isimpendelee Chatanda kwani sisi tumebaini huyu mama hatufai,”alisema Bananga.
0 comments:
Post a Comment