WAMACHINGA WAVURUGA AMANI JIJINI MWANZA

Wednesday, 6 July 2011

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
amanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro (mwenye kofia nyeusi) akielekea eneo la tukio kutoa amri ambayo kwa kiasi ilirejesha amani baada ya vurugu kushamiri.
Leo kuanzia majira ya saa 3:10 asubuhi kumezuka vurugu jijini Mwanza kati ya wafanyabiashara ndogo ndogo al-maarufu kama Wamachinga na Jeshi la Polisi Mwanza kwa wafanyabiashara hao kudai kufukuzwa eneo lao la biashara tofauti na makubaliano, hali iliyosababisha watu kaadhaa kujeruhiwa na wengine watatu kuhofiwa kupoteza maisha.


Magari mawili ya mfanyabiashara maarufu mkoani hapa Mukeshi vunja bei yamechomwa moto na kuteketea, vibanda kadhaa vimevunjwa, Baadhi ya bidhaa zilizopangwa nje zimeibiwa nayo matairi yamechomwa katikati ya njia panda kuingia mtaa wa Makoroboi kuelekea Soko kuu na kiunganishi cha barabara ya Lumumba Mwanza huku baadhi ya wamachinga hao wakirusha maboksi yaliyoshika moto kwenye majengo yaliyo karibu na eneo hilo kwa nia ya kuyachoma moto.
Vibaka wamepora bidhaa na mali zilizokuwa nje ya Nono Super market na kisha kuchoma friji lilokuwa na vinywaji ambavyo walivinywa kabla ya kuliteketeza.
Kusanyiko la shaka-shaka.
Matairi pia yamechomwa mbele ya lango kuu la soko kuu la jijini Mwanza hali iliyopelekea kufungwa kwa soko hilo nazo biashara kusitishwa.


Friji likiteketea kwa moto.

0 comments:

Post a Comment